Jamani huyu mtu nilijua ni sanamu ila haikuwa kweli kama sanamu,niliposogea karibu mambo yalikuwa tofauti kabisaa,nilipompa mkono jamaa akaupokea..
Kumsalimia akaikubali salamu kwa wema na heshima zote..ila niliangalia chini niligundua kumbe jamaa ni staili yake ya kuomba pesa kijanja.
Mwisho nikampa tano na yeye akanipa tano na mambo yakawa mswano,kweli tembea uone
Burudani ya leo ni pale nilipokutana na wabongo nchini Holland,yani ilikuwa raha sana kwa kubadilishana mawazo...kutoka kushoto ni ndugu Jeffy,Othman (Zagaza) shekh Hija,Nico na bwana Naweza` ambao nilikutana na wabongo hao wakifanya mazoezi ya viungo katika kujiweka miili yao vyema kiafya.
Aisee ilikuwa raha ya ajabu baada ya kila mmoja wetu kupewa nafasi ya kutoa mada ambazo zilikuwa muhimu sana katika maisha yetu sisi vijana tunaoishi majuu.tulizungumzia mambo mengi sana na yenye msingi wa maendeleo kwa ujumla.hapo shekh Hija alikuwa akisisitiza jambo fulani kwa vitendo na kila mmoja alikuwa makini kumsikiliza.
Akaja ndugu yetu bwana Naweza` nae alizungumza mambo mengi sana yenye msisimko mzuri kwa vijana wenye umri wetu na matendo yetu.kwa kweli kila mmoja alifurahia mazungumzo yetu.
0 Comments