Mwanasoka wa timu ya Bolton ya Uingereza ,Fabrice Muamba ambaye alipata tatizo la moyo wake kusimama alipokuwa uwanjani akichezea timu yake, amepata ruhusa ya kwenda nyumbani.
Muamba ambaye alikuwa akipata matibabu katika hospitali ya moyo mjini London. Kiungo huyo wa Bolton Wanderers alianguka uwanjani wakati klabu yake hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya Tottenham katika mchezo wa robo fainali ya kombe la FA tarehe 17 Machi.
Muamba amewaambia waandishi wa habari kwamba anatarajia kupata muda na familia yake huku akiwarudishia shukurani mashabiki na wenzake ambao waliungana naye wakati wote akiwa hospitalini.
Hapo Jumamosi shirikisho la soka Italia lilisimamisha mechi zote baada ya mchezaji wa klabu ya Livorno, Piermario Morosini, kuzirai na baadaye kufariki dunia alipokuwa akichezea klabu yake.
0 Comments