Na Hamida Hassan
MAMA mzazi wa Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtagoa amemzungumzia msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayetuhumiwa kuwa ndiye chanzo cha kifo cha mwanaye na kusema yeye hawezi kumchukia kwani anaamini kilichotokea ni mipango ya Mungu.
Akipiga story na chanzo cha habari hizi nyumbani kwa marehemu, Vatican Sinza alisema kuwa yeye kwanza hamjui Lulu na wala hajawahi kukutana naye, wala hakuwahi kujua kuwa ana uhusiano na mwanaye kwa sababu hakuwahi kupewa utambulisho.
“Namshukuru Mungu ingawa inauma na ni vigumu kuamini lakini siwezi kumlaumu wala kumchukia mtu, ninachoamini Mungu amempenda zaidi mwanangu na amekufa kama wanavyokufa wengine,” alisema mama huyo kwa masikitiko.


Enzi hizooooooo za uhai wake Steven Kanumba alipokuwa akimfundisha Lulu namna ya kucheza movie.Rest in Peace msanii wetu uliyevutia wengi katika uigizaji wako.Utabaki kuwa gumzo maishani.