RCO JOSEPH KONYO SSP AKIITOLEA UFAFANUZI SIRAHA HIYO.
KAIMU KAMANDA KIHENYA KIHENYA AKIWAONESHA WAANDISHI WA HABARI SIRAHA MBILI ZA KIVITA AINA YA SMG ZILIYO KAMATWA

Na Pardon Mbwate na Felister Elias wa Jeshi la Polisi -KigomaKIGOMA IJUMAA APRILI 13, 2012. Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma linawashikilia watu wanne wakiwemo wawili raia wa nchi jirani ya Burundi kwa tuhuma za kupatikana na silaha mbili za kijeshi aina ya SMG na risasi mbili.Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya wa Kihenya, amewataja Raia hao wa Burundi waliokamatwa kuwa ni Ndolimana Alfred Ndoli(29), mkaazi wa Lutana Kiharu na Bosco Yohana Gabriel(35), mkaazi wa Kibimba Giharu ambao walikamatwa katika kijiji cha Nguruka silaha moja wakiwa na SMG moja yenye namba 56–2500509Kamanda Kihenya amewataja Watanzania waliokamatwa sambamba na Warundi hao kuwa ni Matata Chubwa Ntasamba(36), mkaazi wa kijiji cha Kitanga Wilaya ya Kasulu na Ndegeya Medard(28), mkazi wa kijiji cha Kitanga wilaya ya Kasuliu mkoani Kigoma walikamatwa katika Kitongoji cha Lugongoni tarafa ya Nguruka wakiwa na magazini mbili za SMG na moja kati ya hizo ikiwa na risasi mbili. Amesema kuwa silaha iyoyo na risasi ilipatikana katika kandokando ya mto Ruguzye uliopo katika pori la kijiji cha mabama wilayani Kinondo baada ya kutelekezwa na majambazi wasiojulikana kufuatia msako mkali unaoendelea mkoani humo wa kutafuta silaha na majambazi wa kutumia silaha. Katika tukio lingine Kamanda Kihenye amesema mkazi mmoja wa Kitongoji cha Mrusi mjini Kasulu, Elizabeth Kanyungu(46), alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani ndani ya nyumba yake.Kamanda Kehenye alisema marehemu alijinyunga majira ya saa 6 usiku kwenye mkesha wa Pasaka wakati familia yake ikiwa kanisani kushiriki ibada ya pasaka. Amesema Polisi bado wanachunguza kupata chanzo na sababu za mtu huyo kujinyonga.Wakati huo huo, mkazi mmoja wa kijiji cha Kasangezi wilaya ya Kasulu Zakayo Nkika(37), alipigwa na wananchi wenye hasira kali hadi kufa baada ya kuwajeruhi watu saba wa kijiji cha Kasangezi wilaya ya Kasulu kwa kuwakatakata kwa mapanga.Marehemu ambaye alielezwa kuwa alikuwa ni mtumiaji wa dawa za kulezwa aina ya mihadarati aliuawa na wananchi hao wakati akiwa katika ofisi ya mtendaji wa kijiji hicho alipokamatwa kwa tuhuma za kuwajeruhi watu saba wa kijiji hicho bila sababu. Kamanda Kihenya amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Vicent Mdadili(30), Linus Joseph(25), Samson Rutabina(45), Shukuru Musunu(30), Kulwa Mathias(27), Rashid Musunu(35) na John Rumie(55) wote wakaazi wa kijiji cha Kasangezi. Majeruhi wote walikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Kasulu kwa matibabu na wawili hati yao ambao ni Samson Rutabina na Shukuru Musunu wameelezwa kuwa hali zao ni mbaya.Kutokana na tukio hilo, kamanda Kihenya amewataka wananchi kuaacha kuchukua sheria mkononi kwa kuwaua watuhumiwa wa makosa mbalimbali kwani amesema kwa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria na ni kosa la jinai.