Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na wajumbe wa chama cha wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa wa nchi ya Brazil alipokutana nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi jijini Sao Paulo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na viongozi wa chama cha wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa wa nchi ya Brazil alipokutana nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi jijini Sao Paulo, katika siku yake ya mwisho ya ziara yake ya Brazil April 19, 2012. Wa pili kulia ni Makamu wa Rais wa chama hicho Bw Joao Guilherme Sabino Ometto na kushoto ni Mkurugenzi wa chama hicho Thomaz Zanotto na kulia ni Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun Ali Suleiman.PICHA
NA IKULU.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 19 aprili amewakaribisha wawekezaji SA Brazil kuja kuwekaza Tanzania kwa minajili ya pande zote mbili kufaidika.
"hatutafuti msaada , tunatafuta uwekezaji ili pande zote zipate faida" Rais amewaambia wafanyabiashara wa Brazil wakati anafungua semina ya siku moja iliyofanyika katika Makao Makuu ya Shirikisho la Wenye Viwanda wa Sao Paulo (FIESP).
Katika semina hiyo, Kituo cha Uwekezaji cha Tanzania, (TIC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kituo cha Eneo Maalum la Uwekezaji (EPZ) wamepata nafasi ya kuelezea kunusuru nafasi za uwekezaji nchini Tanzania.
Nafasi hizo ni kwenye Kilimo, Utalii, Miundombinu, Usafiri wa Anga, Bandari na maeneo kadhaa yakiwemo ya huduma.
Mapema tarehe 18 April, Rais Kikwete amepata nafasi ya kutembelea ofisi za Shirika la Chakula Duniani (WFP) na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Bw.Daniel Balaban na kupata maelezo kuhusu jitihada ya kituo hicho ,ambacho pia kinafanya jitihada za ziada kupambana na njaa nchini Brazil.
Kupitia kituo hicho, Brazil inasaidia nchi mbalimbali kupambana na njaa na tayari juhudi hizo zimeanza kuisaidia Tanzania ambapo wataalamu wa Brazil watatembelea Tanzania na watanzania watatembelea Brazil kwa ajili ya semina zenye lengo la kuwapa utaalamu na mbinu za kupambana na njaa.
Kupitia WFP Brazil, Tanzania pia itafaidika na mpango wa kutoa chakula kwenye shule za msingi ili kuongeza mahudhurio ya watoto shuleni na pia kuwapa utulivu wa kuweza kuhudhuria na kupenda masomo.
Leo Rais Kikwete amekamilisha Ziara yake Kwa kutembelea kampuni Kubwa inayotengeneza ndege za biashara na kijeshi cha EMBRAER .
Rais kikwete anaondoka usiku wa leo 19 aprili kurejea nyumbani na anatarajia kuwasili nchini tarehe 21 aprili mchana.
                                                     ...................mwisho..............

          Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi Habari wa Rais, Msaidizi,Sao Paulo, Brazil,19 Aprili, 2012