Hapa nilipokuwa nchini Holland wakati navuka kivuko cha serikali kwenda ng`ambo upande wa pili kwa rafiki yangu kamanda Kiseke sikuchajiwa hata senti tano,yani ilikuwa ni free kwenda na kurudi na ndio system ya wenzetu maana wanajua kuwa kuna wakazi ambao wanafanya shughuli zao ng`ambo ya pili na wakichajiwa nauli kila trip inakuwa wakati mgumu sana kimaisha kwa mwananchi.kiukweli niliupenda sana utaratibu ule wa serikali kwa kujali hali ya mwananchi wa kipato cha chini,suala la upatikanaji wa petrol ya hicho kivuko ni juu ya kodi ya mwananchi na sio .................
Kwa Tanzania hali sio sawa na wenzetu na hapo swali linapokuja toka kwa wazungu wanapotuuliza kwanini tunawachaji wananchi kwa kuvuka upande wa pili na hicho chombo ni cha serikali mimi binafsi huwa sina jibu la kumridhisha muulizaji hubaki utaratibu wa kwetu na wa kwenu ni tofauti,yani huwa nakufa na tai shingoni wallah.ila naamini kila jambo huwa na mwanzo na mwisho wake,Mungu Ibariki Afrika.
0 Comments