Wananchi wa Ufaransa wanapiga kura kwenye uchaguzi wa rais ambao wengi wanaona kuwa ni kura ya maoni juu ya uongozi wa Rais Nicolas Sakorzy.
Wagombea tisa wanampinga Rais Sakorzy, pamoja na Francois Hollande, wa chama kikuu cha upinzani, chama cha kisoshalisti.

Vyama vya mrengo wa kushoto zaidi na kulia zaidi vimefanya kampeni kali piya.

Waandishi wa habari wanasema uchaguzi unafanywa wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu uchumi, lakini inaelekea siyo watu wengi watajitokeza kupiga kura katika duru hii ya kwanza.

Washindi wawili wa leo watapambana tena kwenye duru ya pili mwezi ujao.