Afrika Kusini imeanza kuweka ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini humo kutoka China.
wadadisi wanasema hii ni ishara ya ushindani mkali wa kibiashara kati ya mataifa ya nchi za Brazili, China na Afrika ya Kusini, zinazojulikana kama BRICS.
Tayari Serikali ya Afrika Kusini imeanza kutoza ushuru kwa kuku wanaotoka Brazil huku nchi hiyo ikitishia pia kuishtaki Afrika Kusini kwenye shirika la biashara duniani.
Utawala wa Afrika Kusini umehofia kwamba bidhaa za nje zitahatarisha nafasi za ajira, huku idadi ya watu wasiokuwa na ajira nchini humo ikifikia asili mia 25.