Basi la abiria la Kampuni ya Muro Investment, lenye nambari za usajiri T 820 BEY lillilokuwa likitokea Jijini Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku jana, haikusababisha madhara kwa abiria isipokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto huo. Basi hili ni la pili kwa kuteketea kwa moto ndani ya wiki hii baada ya Basi la Sumry kuteketea kwa moto Mkoani Dodoma.Picha na Father Kidevu Blog.
Wakazi wa Maseyu na wasafiri wakiangalia basi hilo likiteketea kwa moto.
Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto. 
 Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo ulioliteketeza basi hilo kabisa.