Mzoefu wa mambo Dj Chilli ndiye mtaalamu atakayezikangaa nyoyo za watu siku hiyo
Hello Everyone..!!
Waungwana wote toka pande zote za Africa,Tanzania,Burundi,Rwanda,Somalia,Kenya na nchi jirani za Africa na Ulaya kwa ujumla.Kwa mara ya kwanza katika kuleta umoja na kushirikiana vyema kama waafrika tumeandaa Buffet Party ili kila mmoja apate kujumuika na kukutana na wenzake.

Kila mmoja ana haki ya kuja na kuburudika na wenzake ili kusukuma maisha.Burudani ya muziki itaanza saa moja na nusu usiku (19hrs) mpaka asubuhi.Vinywaji na chakula vinapatikana bureee(soft drinks)mambo mengi yatapatikana siku hiyo kwa wale wote watakaokuja ukumbini hapo,kwa wacheza poll,Darts na mengineyo wataburudika vya kutosha.

MAHALI- LEUVEN

Ukumbi upo Leuven na unajulikana kwa jina la`` Pocket level one``na anuani yake jinsi ya kufika  JP minckelerstraat 98, te 3000 Leuven, Kiingilio ni sawa na bure.kila mmoja atalipa euro 10 tu na kila kitu ndani ya ukumbi atapewa buree kuanzia vyakula mpaka vinywaji baridi.

TAREHE
02/06/2012 Siku ya Jumamosi
                                                         
MUHIMU
Mavazi yaliyo mazuri,Ugomvi au Fujo aina yoyote haitaruhusiwa.Kuwahi ukumbini ni suala la msingi,na kwa yoyote ambaye itakuwa ngumu kwake kufika ukumbini namba za simu zitakuwekwa siku za usoni.tunaomba watu wote mje kwa wingi ili tuburudike kwa pamoja na kwa yoyote atakayeona tangazo hili tunaomba tafadhali awajulishe na wenzake.