Na Shakoor Jongo
SUPASTAA wa muvi za Bongo aliye pia Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu (pichani juu) anaonekana kuanza kuonja machungu ya kuwa na uhusiano wa kimpenzi na mume wa mtu.
Madai yanasema Wema anakumbana na kadhia hiyo kwa vile anashindwa kulala naye kwa uhuru mwanaume huyo na kumfanya aumalizie usiku akiwa na midoli kitandani.
Itakumbukwa hivi karibuni, Wema aliripotiwa kufanyiwa fujo na mwanamke aliyedaiwa ni mke wa mwanaume anayetoka naye kimapenzi kwa sasa ambaye alipata taarifa za usaliti wa mumewe.
Hata hivyo, katika picha za staa huyo za hivi karibuni, anaonekana amelala kitandani akiwa amekumbatia midoli, hali inayoashiria kuwa upweke umemsonga kuliko zamani.
Picha hizo zilipigwa miezi michache tu baada ya picha nyingine alizopiga akiwa amelala na aliyekuwa mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’ enzi za utamu wa mapenzi yao.

KAULI ZA MASHOSTITO
Baadhi ya mashoga wa staa huyo walioongea na gazeti hili walikiri Wema kulala mwenyewe jambo ambalo walisema linampa unyonge sana.

KWA NINI?
“Kwani hamjui kuwa jamaa yake wa sasa ni mume wa mtu? Kwa hiyo hata akiwa kwa Wema, mwisho saa sita au saba, anakwenda kwa mkewe.


“Wakati ule akiwa na Diamond walikuwa wanajiachia, hakuna aliyekuwa akimuuliza amelala wapi wala alikwenda wapi?” alidai shosti mmoja ambaye aliomba hifadhi ya majina yote.
Shoga mwingine wa Wema ambaye amekuwa akizagaa naye sehemu kadhaa za Jiji la Dar, alipoulizwa kuhusu upweke wa msanii huyo alisema:
“Inawezekana hiyo hali inamsumbua, hata mimi siku ‘nikigombanaga’ na wa ubani wangu, napata tabu kulala mwenyewe, kwa upande wa kuwa na mume wa mtu kwa kweli hana msaada kwa usiku ukiwa kitandani maana yeye anakuwa kwa mkewe.”

WEMA ANASEMAJE?
Wema mwenyewe alipobanwa na mwandishi wetu alikanusha vikali madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wa mtu.
Ijumaa: Khaa! Sasa mbona kuna kipindi iliripotiwa kuwa una uhusiano wa kimapenzi na mume wa mtu hadi ikatokea mkewe akakufanyia fujo pale Kinondoni, leo unakanushaje Wema?
Wema: Kwanza nakuomba ufute kauli yako ya kwamba mimi nina uhusiano wa kimapenzi na mume wa mtu, ningekuwanaye ningejaza midoli kitandani?
Ijumaa: Oke, kwa hiyo unataka kuniambia hiyo midoli ndiyo inayokufariji kwa sasa ukiwa kitandani?
Wema: Tena sana, ila itafika kipindi nitapata ninayemuona ni chaguo langu na nitamuweka hadharani, yanini nimfiche kama wengine wanavyoficha mabwana zao?
Ijumaa: Je, ikiwa huyo unayesema ndiye atakuwa chaguo lako kama ni mume wa mtu utathubutu kumuweka hadharani?
Wema: Sasa nimfiche wa nini, yeye anajijua kuwa ni mume wa mtu kwa nini anifuate? Nitamuweka hadharani akigombana na mkewe mimi hilo silijui ni yeye na familia yake.