MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya mjini The Hague, imemhukumu kifungo cha miaka 50 jela aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor.
Baada ya kesi iliyodumu miaka sita, Taylor alipatikana na makosa kumi na moja ya kufadhili na kusaidia waasi nchini Sierra Leone, ili apate madini ya almasi.
Taylor ni kiongozi wa kwanza wa zamani kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa tangu kumalizika kwa vita vya pili.
Raia wa Liberia wakishangilia kwa mabango baada ya kusikia matokeo ya hukumu kwa aliyekuwa Kiongozi wa nchi hiyo miaka iliyopita bwana Charles Taylor.
0 Comments