Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Haruna Masebu
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza kupungua kwa bei ya mafuta ya nishati jambo linaoonyesha kuwapo kwa unafuu.Bei petroli imepungua kwa asilimia 2.16 na dizeli kwa asilimia 2.59 kuanzia leo.Mkurugezi wa Ewura, Haruna Masebu alisema jana kuwa hii ni sawa na punguzo la Sh48 kwa petroli na Sh 54 kwa dizeli. Punguzo hilo limetokana na mabadiliko ya bidhaa hiyo katika soko la dunia.Masebu alisema pamoja na kushuka bei katika soko la dunia pia gharama za usafirishaji na faida kwa kampuni inayoingiza mafuta nchini imepungua kwa wastani wa tani asilimia 51.71 kwa mafuta ya petroli na dizeli ni kwa silimia16.13 na kwamba nayo shilingi ya Tanzania imeimarika kwa asilimia 0.34 dhidi ya Dola ya Marekani.“Bei ya jumla kwa petroli ni Sh 48.28 kwa lita ambayo ni sawa na asilimia 2.24 wakati dizeli ni Sh 54.39 kwa lita ni sawa na asilimia 2.69. Lakini kwa bei za rejareja petroli ni Sh 48 kwa lita sawa na asilimia 2.16 na dizeli ni Sh 54 kwa lita ni sawa na asilimia 2.59, lakini mafuta ya taa bei yake haijashuka wala kupanda,” alisema Masebu.Masebu alisema kwa mujibu wa sheria ya mafuta ya mwaka 2008, bei ya mafuta ya petroli itaendelea kupangwa na soko hivyo Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo ikiwa ni lengo la kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuaji wa mafuta.“Kampuni za mafuta zipo huru kuuza mafuta ya petrol kwa bei ya ushindani ili mradi bei hizo ziwe chini ya bei kikomo kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na Ewura na ambayo ilichapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 454 la Desemba 23, 2011” alisema Masebu.Alisema vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na wateja.“Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayooonekan vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika”, alisema.Alisema wanunuzi wote wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.Alisisitiza kwamba stakabadhi hizo zitatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei ya kikomo ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.
0 Comments