Pichani Brother Hasheem aliyeketi kushoto na mimi niliyekunja miguu tulikuwa tukipiga stori siku za hivi karibuni nyumbani kwake Den Haag.


Kati ya tabia 117  nilizorithi kutoka kwa wazazi wangu ni tabia moja ambayo naipenda ya kumsifia mtu akiwa hai.wazazi wangu walikuwa wakipenda sana kumpa sifa mtu akiwa hai,na wanapomsifia huwa wanamsifia mtu kiukweli bila unafiki.

Sikuona vibaya kuchukua baadhi ya tabia nzuri kutoka kwa wazazi wangu.Leo nitachukua fursa ya kumsifia Brother Hasheem mkazi wa kitongoji cha Den Haag nchini Holland.Ni miaka michache tangu kujuana nae ila amekuwa na sifa nyingi kabla ya kukutana nae,ni mmoja wa watu wenye hekima na busara kwa watu wa rika zote,mcheshi,mkarimu na mtu mwenye upendo kwa watu.

Brother Hasheem ni mmoja wa watu ambao kwa upande wangu namchukulia kama mtu mmoja simple sana anayekubalika katika kila mahala ukilinganisha na baadhi watu ambao tabia zao huwa hazitabiriki machoni mwa watu.

Kingine ambacho nakipenda toka kwa brother Hasheem ni kwamba hana majivuno na ni mtu ambaye ana tabasamu kila unapokutana nae.Kingine ambacho nimejifunza kwake ni kwamba tabia hii ya ucheshi wake sio tu kwake mpaka kwa mkewe.sio siri Mungu awajaalie kwani tabia yao binafsi naipenda sana.

Ni kitu kigeni sana kwa wanadamu wa sasa kufikiria ninavyofikiria mimi,ila kwa upande wangu naona ni kitu cha kawaida kumsifia mwenzangu kwa uzuri alionao kimatendo,nafsi na utu,huwa sipendi kumsifia mtu akiwa ametangulia mbele ya haki.nimeonelea nianze utaratibu huu kila nipatapo nafasi ya kumsifia yule ambaye naona kwa upande wangu anastahili sifa.

Brother Hasheem Mungu akujaalie kwa wema wako na utu ulionao wewe na mkeo hapo mlipo,kwa upande wangu mnastahili pongezi za dhati toka kwangu.
Nawatakia Ijumaa njema na Mungu awalinde na mabaya na kuwanyooshea mazuri.

Ujumbe wangu kwa waungwana.
Msifie mtu kwa uwezo wake aliojaaliwa na Mungu,tuache ile kasumba ya kupondana,kuna watu wana nyota zao ambazo zinastahili kung`ara na hiyo ndio kudra aliyojaaliwa hivyo tukubaliane nayo.

Tuache tabia ya kusifiana pindi tukifa,au tabia ya kuoneana choyo...
                                                                    Maganga One.