Waendesha mashtaka katika kesi ya rais wa zamani wa Liberia Charles Charles Taylor, wameomba adhabu ya kifungo cha miaka 8 jela itolewe dhidi yake.

Bw Taylor alipatikana na hatia ya makosa ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa mjini The Hague, wiki iliyopita.

 
Katika pendekezo lao lililowasilishwa mbele ya mahakama hiyo maalum inayosikiza kesi ya Seirra Leone, waedesha mashtaka walisema hukumu hiyo inamfaa kutokana na uzito wa uhalifu wa kivita alioufanya bwana Taylor.


makosa


Mahakama hiyo inayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa ilimpata bwana Taylor na hatia ya kuuga mkono makundi ya waasi waliofanya mauaji ya kikatili, ubakaji, na kukata viungo vya binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka kumi na moja nchini Sierra Leone.

Kiongozi huyo wa zamani wa Liberia anatarajiwa kuhukumiwa Mei 30.

Mahakama hiyo haitoi hukumu ya kifo.  BBC