Mkurugenzi Mkuu Charles Ekelege wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) |
Mkurugenzi huyo anakabiliwa na tuhuma za kuanzisha kampuni hewa za ukaguzi wa magari nje ya nchi hususani, Hong Kong na Singapore na kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya fedha.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Abdallah Kigoda alithibitisha hayo jana alipokuwa anaelezea mikakati yake mipya ya kiutendaji tangu ateuliwe na Rais Jakaya Kikwete kuiongoza wizara hiyo hivi karibuni, akichukua nafasi ya Dk Cyril Chami.
“Kashfa ya TBS ni moja ya sababu za kupanguliwa kwa wakuu wa wizara, hivyo kwa kuanzia, nimeiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya TBS kumsimamisha kazi Ekelege ili kupisha uchunguzi ndani ya shirika hilo,” alisema Dk Kigoda.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya TBS, Oliver Mhaiki alipoulizwa juu ya taarifa hizo, alisema hajapokea maagizo ya Waziri. Aliongeza kuwa, katikati ya wiki ijayo kutakuwa na kikao cha dharura cha Bodi kuzungumzia mambo kadhaa yanayohusu utendaji wa shirika hilo.
“Mara tukipokea taarifa rasmi juu ya suala hilo kutoka wizarani, tutaliingiza katika ajenda zetu za kikao,” alisema.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Abdallah Kigoda |
0 Comments