Taarifa za vyombo vya habari vya Kuwait zinaeleza kuwa jopo la mahakama limemhoji waziri mkuu wa zamani, Sheikh Nasser al-Mohammad al-Sabah, kuhusu tuhuma kuwa alighushi dola mamia ya mamilioni na kuziweka kwenye akiba zake za benki nchi za ng'ambo.

Sheikh Nasser, ambaye alijiuzulu mwezi wa Novemba, anakanusha tuhuma hizo.
Vyombo vya habari vya Kuwait, vinaeleza kuwa aliyerithi nafasi ya Sheik Nasser, Sheikh Jaber Mubarak al-Sabah, amezungumza mbele ya jopo la bunge linalochunguza kisa hicho piya.
Viongozi wote hao wawili ni wa ukoo ulioongoza Kuwait kwa zaidi ya karne mbili na nusu.