Mama Salma Kikwete Mke wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya STAND UP FOR AFRICAN MOTHERS iliyoandaliwa na AMREF ambapo aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto wao wakati wa kujifungua, Mama salma alisema kuwa kila mwananchi akichangia Sh.1000 za kitanzania, zitasaidia kusomesha wakunga 4222 watakaotumika kuwauguza wamama wajawazito pindi wanapokuwa kwenye kipindi cha kujifungua, Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Dk Hussein Mwinyi akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi huo ambapo aliitaka Amref isaidie kukusanya pesa kutoka kwa nanchi pamoja ana Makampuni Binafsi ili fedha za kusomesha wakunga zipatikane.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Amref wakisherehekea kwenye uzinduzi huo.
Mama Salma Kikwete akimpongeza Mkurugenzi mkuu wa Amref Dk Festus Ilako kwa kuonyesha upendo kwa kinamama wajawazito.
Kikundi cha Burudani kutoka Mjomba Band kikifanya mambo kwenye Uzinduzi huo.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
0 Comments