Pichani kushoto ni mlezi wa kijana aliyeketi katikati ambaye siku hii alikuwa akifanya kisomo cha kumrehemu mzazi wake aliyetangulia mbele ya haki mzee Amiri Khamis Hassan.
Hata upande wa kina mama walikuwa wakiendeleza dua na mawaidha kwa marehemu mzee Amiri Khamis Hassan.
Kwa umakini zaidi wageni toka nchi mbalimbali walikuwa wametulia wakisikiliza mawaidha yaliyokukuwa yakitolewa siku hiyo.
Mama wadogo waliotoka nchini Holland walifika katika kisomo hicho nchini Ubelgiji kujumuika na kina mama wengine.
Mtoto wa marehemu Amiri Khamis Hassan akifarijiwa na watu wa mataifa mbalimbali siku ya kisomo hicho
Kiukweli kisomo kilikwenda vizuri na kwa niaba ya familia nzima ya mfiwa tunawashukuru watu wote waliojitolea kwa hali na mali kufanikisha kisomo hicho na hata waliokuwa na nia ya kuja wakashindwa kufika kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao nao Mungu atawalipa.
                          KWA PICHA ZAIDI KWENYE KISOMO HICHO
                                                            BONYEZA HAPA