Stori na Shakoor Jongo na Musa Mateja STAA mcharuko katika tasnia ya filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ hivi karibuni alikuwa hoi na kulazwa hospitalini akisumbuliwa na ugonjwa usiokubalika wa malaria.
Chanzo cha habari kilipata taarifa za kuugua kwa msanii huyo Mei 23, mwaka huu ambapo katika kufuatilia ikagundulika ni kweli na alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Sandarya iliyopo Kijitonyama jijini Dar.
Akizungumza kwa tabu, Jini Kabula alisema alikuwa akijisikia vibaya siku nyingi zilizopita akawa anapuuzia lakini siku hiyo akawa amezidiwa hivyo kukimbizwa hospitalini hapo na kulazwa.
“Nilihisi kuumwa muda mrefu, nikawa napuuza sasa jana ndiyo nikazidiwa na kuletwa hapa hospitalini,” alisema Kabula.
Alisema baada ya kufika hapo alitundikiwa dripu za dawa ya Quinine mfululizo na kwamba alikuwa akielekea kupata nafuu.