Aisee hii keki yangu peke yanguuuu au na nyie mnaisubirii? maneno ya Nabil hapo jana akiwa anamuuliza rafiki yake wa pembeni.
Kwikwii kwii kwii..kwaaa kwaaa kwaaa Nabil weeee zima mishumaa hiyoooooooo......!!!!!!!
Baada ya kuzima mishumaa kama kawaida mzaa chema alisogea karibu na kumsaidia kijana wake Nabil jinsi ya kukata keki..
Kula mwanangu,kula kijana wangu,kula handsome boy wangu kula ukue mwanangu na ukue nikutume mwanangu.
Baada ya kulishwa keki na mama yake mzazi kijana Nabil aligeukiwa upande wa pili na kusema mama mzaa chema kula kipande hiki cha keki na Mungu akubariki kwa malezi unayonipa.
Baada ya kumlisha keki mama mzazi kijana Nabil aligeukia upande wa nyuma na kusema namlisha keki dada yangu wa kwanza kunitangulia..
Kijana Nabil akurudi kwa chini na kusema zamu ya mdogo wangu sasa kula keki..
Na hapa ni zamu ya rafiki yake kipenzi Denzel washington kulishwa keki... |
Pichani kijana Nabil akipokea zawadi ya baiskeli aliyenunuliwa na uncle wake pichani.
Nabil akipokea zawadi toka kwa mama Yannis
Hii ndio familia nzima ya Nabil,yani hapo Baba,Mama,Dada,Nabil mwenyewe na mdogo wake mdogo aliyebebwa na mama yake.Allah awafanyie wepesi kwa kila jambo lao jema na awalinde na mabaya insh`Allah amen.
Hapo ni uma kwa vijiko mdomoni kwa kwenda mbele....toa wali weka nyama....
Wageni waalikwa wakivunja mifupa kama kawaida....
Hawa ni wazazi wa Nabil nao walijumuika na wageni waalikwa kwenye mambo ya maakuli...mama Nabil akifurahi kwamba mtoto wao sasa ni kidume cha Liverpool siku za usoni.
Kama wakaida yetu kwenye shughuli za sherehe basi huwa hapakosi madikodiko na kama unavyojionea kila mmoja samahani ilipendeza
Na hapa wageni waalikwa wakiwa wametulia vizuri kufuatilia nini kinaendelea kwenye shughuli ya kuzaliwa kwa kijana wetu Nabil |
Mduara nao ukashika nafasi yake...
Yani palikuwa hapatoshi kwa kiduku
Hapo chacha....
Kila mmoja yupo bize na muziki
Nice One
Kwa raha zetu weraaa weraaa aaaaa
Wacha weeeeeee kweli kila mtu na mtuwe
Kijana Nabil akiwa na madada zake walipata flash kuweka mambo sawa....
Mduara ukiendelea kama kawaida mwenye kuramba aliramba mwenye kustua kijoti alistua basi ilikuwa Wera weraaaaaa mambo mswano. |
Na ukurasa ukafungwa na Mrs Eddy a.k.a Fatuma Mashauzi Classic ambaye ujumbe wake ilikuwa ni ``AMANI na UPENDO kwa kila mwanadamu ndio msingi wa mafanikio...``na kuwatakia kila la heri watoto wote duniani na kina mama wenzake.
2 Comments
What web host are you using? Can I get your affiliate link to your
host? I wish my web site loaded up as quickly
as yours lol
Also visit my weblog gerber whole life insurance