Naibu Mkurugenzi wa michezo, Bi. Juliana Yasoda (kulia) akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti, Bw. Ephraim Mafuru (kati) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Masiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula (Kushoto). Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Sunday Kayuni (pili kushoto) na kocha msaidizi wa Twiga Stars Bi. Nasra Mohamed.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB Bw. Imani Kajula alisema; NMB imekua mbele katika kuchangia soka Tanzania, leo hii NMB ikishirikiana na Serengeti tunachangia maandalizi ya Twiga Stars”.

NMB inatambua kuwa Twiga Stars ikiwezeshwa inaweza ikafanya vizuri zaidi. Ili kutimiza lengo hili, NMB Ikiwa ndiyo benki yenye mtandao mpana wa matawi mengi Tanzania nzima pia imeanzisha akaunti maalum kwa ajili ya kuchangia Twiga Stars. Yeyote atakayeguswa kuchangia Twiga Stars anaweza kuchangia kupitia akaunti namba 22310001185 yenye jina CHANGIA TWIGA STARS ACCOUNT
Katika kuendeleza soka Tanzania, leo hii Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya Bia ya Serengeti imesaidia maandalizi ya Twiga Stars kwa kutoa jumla ya shilingi Milioni Thelathini. Pia NMB na Serengeti wamekabidhi vifaa vyenye thamani ya Milioni Tano kwa timu hiyo ya Twiga Stars.