Washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 wakiwa ICC
Mahakama ya kimataifa inayosikiliza kesi za jinai imepinga rufaa ya Wakenya wanne mashuhuri wanaokabiliwa na tuhuma za kuchochea ghasia baada ya uchaguzi wa mwaka 2008.

Washukiwa hao wanne walihoji mamlaka ya mahakama hio kwa misingi ya kitaalamu.

Uwamujzi huu una maana kua watahukumiwa huko the Hague kwa madai ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Wakenya hao wanne ni pamoja na Mawaziri wa zamani Uhuru Kenyatta na William Ruto --ambao wamekanusha kuwajibika na umwagaji wa damu kufuatia uchaguzi uliosababisha ubishi mkubwa.

Msemaji wa mahakama hiyo Fadio el Abdallah alisema kuwa hoja ya uwezo wa mahakama hiyo kisheria kusikiliza kesi za Kenya, ni swali la kisheria na mahakama imefanya uchambuzi wa swali hilo kwa msingi wa ni nini hasa ukiukwaji wa haki za binadamu na namna ambavyo swala hilo linatazamiwa.


Abadallah ameongeza kuwa mahakama iliamua kwamba hoja za washtakiwa hazikuwasaidia katika kesi zao, bali zilienda kinyume na matarajio yao.

Aliongeza kuwa mahakama ya rufaa ilisema hoja za mawakili wa washukiwa hazihusu uwezo wa mahakama kuendesha kesi hizo bali ni maswali yatakayoamuliwa na mahakama kwa misingi ya uzito wa kesi yao. Na kwa hilo mahakama ikapinga hoja yao.