Sudan imewaondoa wanajeshi wake kutoka eneo la mpaka na Sudan Kusini ambalo linazozaniwa la Abyei. Hii ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi wanaolinda amani eneo hilo wamesema wanajeshi wa Sudan waliondoka Jumanne usiku.
Kuondolewa kwa wanajeshi hao kunatokea wakati Sudan na Sudan Kusini wakianza mazungumzo ya amani kufuatia migogoro ya karibuni.
Mazungumzo ya sasa yanaendelea nchini Ethiopia.Abyei inashindaniwa na nchi mbili, Sudan na Sudan Kusini ambayo ilipata uhuru waka mwaka 2011 kufuatia miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Maelfu ya raia walikimbia makaazi pale wanajeshi wa Sudan walipotwaa eneo hilo kufuatia makabiliano makali na wanajeshi wa Sudan Kusini.Hadhi ya Abyei ingali kuamuliwa na kura ya maoni kuamua hilo imeahirishwa.
Maafisa wa Sudan wamesema wanajeshi wake wameondolewa ili kufanikisha mazungumzo ya amani.
Mazungumzo ya Ethiopia yanatarajia kuangazia masuala kadhaa ikiwemo suala la Abyei.Kuna hisia kali kutoka nchi mbili kuhusu Abyei.
Jamii ya Misseriya, wenye asili ya Sudan na wafugaji hutegemea eneo hilo kwa malisho. Hata hivyo jamii ya Dinka Ngok ambao ni wenyeji wanataka eneo hilo kuwa katika Sudan Kusini.
0 Comments