Raisi mteule wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Duniani (AIWJ), Mheshimiwa Jaji Eusebia Munuo, (katikati) akisikiliza kwa makini wajumbe wengine wakichangia mada kwenye Mkutano huo, mara baada ya kukabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa Raisi wa Chama hicho.
Ujumbe wa Majaji na Mahakimu kutoka Tanzania, wakiwa kwenye picha ya pamoja, mara baada ya kukabidhiwa rasmi Bango la Chama hicho cha Majaji Duniani(AIWJ) na kupewa nafasi ya kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu ujao wa Chama hicho utakofanyika Mwezi Mei, 2014 Mjini Arusha – Tanzania.
Raisi Mteule wa Chama cha Majaji na Mahakimu, Mhe. Eusebia Munuo akikabidhiwa Bango na aliyekuwa Raisi wa Chama hicho, Lady Brenda M. Hale.
Sherehe, nderemo na vifijo katika Ukumbi wa Mikutano, mara baada Mheshimiwa Jaji Munuo kutangazwa rasmi kuwa Raisi mpya wa Chama hicho na Tanzania kukabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa Mwenyeji wa Mkutano ujao wa Chama hicho Mwaka 2014.
Chama cha Majaji Wanawake duniani (IAWJ) kilikuwa na mkutano wake Mkuu uliofanyika London Uingereza tarehe 2-5 Mei 2012.

Kwenye Mkutano huo Tanzania, iliwakilishwa na Majaji na Mahakimu ambao ni wanachama wa IAWJ (International Association of Women Judges) na Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (TAWJA).

Katika mkutano huo, viongozi mbalimbali walichaguliwa kushika nyadhifa kukiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka miwili.

Mhe. Jaji Eusebia Munuo, ambae pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania alichaguliwa kuwa Rais wa chama hicho.

Pamoja na kuchaguliwa ktk nafasi hiyo,Mheshimiwa Jaji Munuo, pia alikabidhiwa rasmi Bango la chama hicho. Kwa kukadhiwa Bango hilo, Tanzania sasa imekabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano mkuu ujao wa chama hicho. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwezi Mei 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC Arusha Tanzania.

Ujumbe wa Tanzania uliokuwepo kwenye mkutano huo ulipokea wadhifa huo kwa shangwe na furaha kubwa kama inavyonekana kwenye picha.

Tanzania itashikilia nafasi hiyo ya Urais wa chama hicho mpaka mwaka 2014.