Waziri wa Nchi (Uwekezaji na Uwezeshaji),Mh. Dk. Mary Nagu akitoa hotuba yake.
Kushoto: Balozi wa Ufaransa Tanzania,Mh. Marcel Escure,Waziri wa Nchi (Uwekezaji na Uwezeshaji),Dk Mary Nagu na Mh. Begum Taj , balozi wa Tanzania Ufaransa
Katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara, ubalozi wa Tanzania ukishirikiana na Jumuiya ya Watanzania waishio Ufaransa wameandaa mkakati maalumu wa kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii pamoja na fursa zake za uwekezaji na biashara.Sherehe hizo zilizoanza Jumanne tarehe 22 Mei 2012 zilijumuisha matukio mawili makubwa yafuatayo:1. Maonyesho ya biashara na utalii2. Jukwaa la Uwekezaji na Biashara (Investment and Trade Forum) Mgeni rasmi katika maonyesho haya ya bishara na Jukwaa la Uwekezaji alikuwa Mh. Waziri Dk. Mary Nagu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mama Mary Nagu aliwaalika Wafaransa kuwekeza katika sekta mbali mbali Tanzania ili kukuza uchumi madhubuti kwa faida ya wanachi wa Tanzania na Ufaransa. Jukwaa hili la Uwekezaji na Biashara ni la kipekee kwa Tanzania hapa Ufaransa katika kutangaza fursa za uwekezaji katika katika sekta mbalimbali zikiwamo kilimo, nishati, miundo mbinu, utalii, madini, na mawasiliano.
Naye Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mh. Balozi Marcel Escure aliwaalika makampuni na jamii ya wafanyabiashara ya Ufaransa kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji Tanzania. Alidokeza kuwa kuna makampuni ya kifaransa zaidi ya ishirini yaliyowekeza Tanzania na mengine yako mbioni kuwekeza.Katika shughuli hiyo, bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania kama kahawa, chai, vinyago, vilionyeshwa. Mwisho Mh. Begum Taj, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa aliwashukuru washiriki na kukaribisha jumuiya ya wafanyabiashara ya Wafaransa kutembelea na kuwekeza Tanzania. katika sekta mbalimbali kama kilimo, nishati, na mawasiliano
0 Comments