Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar, kulia akiwa na Mwana mitindo maarufu Washington DC (Kwetu Fashion Design) Missy Temeke, kwenye Tamasha la usiku wa Africa (African night dinner gala) siku wa jumatano Mei 24,2012 ndani ya ukumbi wa J.W Marriott Hotel,  Mei 24,2012 ndani ya Washington Dc

Tamasha hilo lilihudhuriwa na wageni wapatao 1000 kutoka mataifa mbalimbali, miongoni mwa wageni hao ni mabalozi 50 wa nchi za Africa hapa Marekani,viongozi wa umoja wa mataifa,wawakilishi wa Nchi zinazotoa misaada Africa,wafanyabiashara,viongozi wa nchi tofauti, na viongozi wa juu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani. Tamasha hilo ni miongoni mwa matamasha makubwa na nyeti hapa Nchini Marekani.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Mhe. Iddi Sandaly kiwa na Mwana mitindo mbunifu wa (Kwetu Fashion Design) Missy Temeke

Msafara wa watu 10 wa Tanzania uliongozwa na Balozi wetu Mwanaidi Maajar, Dkt Asha-Rose Migiro,Viongozi wa Ubalozini ,Mwenyekiti wa DMV, Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Mhe. Iddi Sandaly  na mwakilishi mrembo ambae ni mwana mitindo  mbunifu  wa mitindo ya (Kwetu Fashion Design) Missy Temeke
Kama taratibu za sherehe hizo zilivyoandaliwa, mabalozi wote 50 waliingia ukumbini wakiwa wamependeza kabisa huku wakishikilia bendera zakuwakilisha nchi zao kitaifa, Miongoni mwa warembo hao walikuwepo Miss Cameroon,Miss Angola,Miss Sierra-Leone ambao wote wameshiriki kwenye mashindano ya Miss universe wakiliwakilisha bara la Africa.
Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar, na mwakilishi wake waliingia kwenye ukumbi  kufuatana na alfabeti za Nchi wanazowakilisha. Tanzania ilitajwa namba 20, Mhe Balozi Maajar akisindikizwa na  Mwana mitindo mbunifu wa (Kwetu Fashion Design) Missy Temeke
Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar

Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar,  na Missy Temeke walivyokanyaga ukumbini, waliamsha,miruzi na makofi yalitanda ukumbini kwa dakika kadhaa. Missy Temeke alikuwa ameshikia Bendera ya Tanzania akifuatana bega kwa bega na Balozi.


Wakaingia ukumbini. Balozi Maajar alivalia Nguo ya kanga ya rangi ya chungwa na koti lake maridadi lanye mchanganyiko wa mishono ya ki-Afrika magharibi, nguo hiyo maridadi  amboyo imedizainiwa na Mwana mitindo mbunifu wa (Kwetu Fashion Design) Missy Temeke nae alivalia nguo ya langi za bendera ya ki-Tanzania iliyotengenezwa kwa mtindo wa  khanga yenye picha ya Rais wa Tanzania Jakaya Mresho Kikwete mbele na picha ya Mwalimu Julius kambarage Nyerere, nyuma ambayo imebuniwa na  (Kwetu Fashion Design) Missy Temeke


Tanzania imependezesha sherehe kabla haijaisha,huu ni usiku wenu,hongereni”.Urembo wa  Kwetu Fashion Design Missy Temeke ulimeremeta jengo zima kiasi kwamba watu walibaki midomo wazi na mate yakiwatoka.



Tumefurahi sana najisikia Very proud of my County maneno hayo yalisemwa na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Mhe. Iddi Sandaly  . “Tanzania juu juu juu zaidi” afisa mwigine wa ubalozi ilisema kwenye ukumbi. “We came, we saw and we conquer.


“Kiongozi mmoja wa msafara wa Watanzania aliiambia blog hii.Missy Temeke vilevile alijiwezea kupata mikataba ya kusona mitindo na kuwashonea nguo za mabalozi wa nchi 4 na Wawekezaji na wafanyabiashara ,wote walipendezewa na kuvutiwa na nguo aliyovaa Balozi Maajar na aliyoivaa yeye mwenyewe.



Wakati mwingine tunahitaji vitu ambavyo vinatuweka sisi wa-Tanzania pamoja,tunahitaji wakati ambao wote tanaweza kuangaliana,tukafurahi pamoja na kusahau tofauti zetu za kisiasa,kikabila, kidini na kimali,wakati ambao sisi wote takajiona kama ni Watanzania tunaohitaji maendeleo juu, na  wakati huo ndio kama ule ambao Nchi yetu imetamba ndani ya taifa kubwa la Marekani.



Kama kuna Nchi iliyotajwa mara nyingi kwenye midomo ya watu usiku wa jumatano basi nchi hiyo ilikuwa ni Tanzania.Ubalozi wetu vile vile ulifanya kazi kubwa kuiwakilisha Nchi yetu kwenye shughuri ile,kwani shughuli ilikuwa si ya mchezo.Nilipomuhoji mwakilishi wa Kimarekani akiwa anatoka nje ya ukumbi baada ya tamasha kuisha alisema ‘Tonight is African night Gala, the show itself was Tanzania daylight.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt Asha-Rose Migiro akitoa hutuba fupi kwenye Tamasha la Africa Day lililoandaliwa na The African Union Vision  Mei 23, 2012 ndani ya ukumbi wa J.W Marriott  Hotel, Washington Dc Ncini Marekani. (Picha Maelezo na Swailivilla.blogspot.com)