Sudan imewaachilia huru wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaotegua mabomu, ambao walikamatwa mwezi uliopita karibu na mpaka wa Sudan Kusini.
Katika sherehe iliyofanywa mjini Khartoum, maafisa hao walikabidhiwa kwa rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, ambaye anapatanisha baina ya Sudan na Sudan Kusini kwa niaba ya Umoja wa Afrika, AU.

Watu hao wane, kutoka Uingereza, Norway, Afrika Kusini, na Sudan Kusini, walikamatwa wakikusanya mabaki ya vita, katika eneo la mafuta la Heglig, lenye mzozo.

Wakijaribu kuchunguza aina ya silaha zinazotumiwa na pande zote mbili.