Katibu Mkuu wa Wizra ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Vuai Iddi Lila akitia Saini kwa niaba ya SMZ na Kulia ni Msaidizi meneja Wa Kampuni ya SOGEA ya Ufaransa kwa kanda Afrika Mashariki Laurent Brouet kwa ajili ya Ujenzi wa Maegesho na Utanuzi wa Barabara za kutulia na kurukia Ndege katika Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar


                                                            Na Talib Ussi Zanzibar



ZAIDI ya b65 Tsh. Zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa Maegesho na utanuzi wa njia za kurukia na kutua ndege katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Zanzibar unaojuilikana ‘Abeid Amani Karume International Airport.’

Hayo yameelezwa katika hafla ya utiaji saini kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Kampuni ya SOGEA kutoka Ufaransa katika Ofisi za Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Malindi mjini Zanzibar.

Katika hafla hiyo katibu Mkuu wa Wizara hiyo Vuai Haji Lila alitia saini kwa niaba ya SMZ na Laurent Brouet ambaye ni msaidizi wa Meneja wa kampuni hiyo kwa kanda Afrika ya Mashariki ndiye aliyeweka saini kwa niaba ya kapuni yake.

Akifafanua juu ya utiaji saini huo Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Issa Haji Ussi alisema pesa hizo ni mkopo kutoka Benki ya Dunia kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (IDA) ambazo ziliombwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Naibu Waziri huyo alifahamisha kwamba kutekeleza ujenzi huo ni kutimiza mikakati ya Serikali ya Zanzibar katika kukuza uchumi na kuongeza uingiaji wa Watalii humu nchini.

Alisema kwamba kukamilika kwa ujenzi huo kutapelekea Ndege nyingi kuingia Zanzibar na wageni kupata nafasi ya kutembelea Nchini jambo ambalo litachochea maendeleo.

“Viwanja vya Ndege ndivyo vinavyotumika sana kwa kuingiza watalii na uwanja wetu ukikamilika tunatarajia kupokea watalii wengi”alisema Ussi ambaye ni Naibu Waziri.

Ussi alisema mbali na kuongezeka Shughuli za Utalii bali na Wananchi wataweza kupata ajira nyingi tokea mwanzo wa ujenzi hadi kukamilika na pale utakapoanza kutoa huduma.

Naibu Ussi alifahamisha ujenzi huo unategemewa kukamilika katika muda wa Miezi 18 na wakandarasi hao watalazimika kukabizi kazi hiyo kwa Serikali ya Mapinduzi kwa matumizi.

Nae Msaidizi Meneja wa Kampuni hiyo kwa kanda ya Afrika Mashariki Laurent Brouet alisema atahakikisha Kampuni yake Inakamilisha ujenzi huo kwa wakati huo ambao umepangwa ili kuondoa Misuguano isiyo yalazima.

“Tutahakiksha ujenzi huu umekamilika kama Mkataba unavyojieleza” alisemanBrouet.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika mikakati ya kuufanya Uwanja wa Ndege Huo kuwa wa kisasa ili uweze kuruhusu kutua ndege nyingi kwa wakati mmoja.