Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita nchini Rwanda (ICTR) imemhukumu Afisa wa zamani wa wanamgambo nchini humo Ildephonse Nizeyimana (Pichani) adhabu ya kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya kimbari yalifayonyika mwaka 1994.
Nizeyimana mwenye umri wa miaka 48 amepatikana na hatia ya kuamuru kuuawa kwa aliyekuwa Malkia wa Kitutsi Rosalie Gicanda na mauaji ya watu wengine kadhaa.
Hata hivyo Mahakama hiyo ya kimataifa imemfutia mashitaka ya ubakaji yaliyokuwa yakimkabili.
Watu takriban 800,000 waliuawa nchini Rwanda wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika muda wa siku 100 kati ya mwezi April na Juni mwaka 1994.
0 Comments