Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak, amehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama mjini Cairo.
Alikutikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya waandamanaji wakati wa ghasia zilizopelekea yeye kutolewa madarakani mwaka jana.
Hakimu Ahmed Refaat alisema watu wa Misri walivumilia miaka 30 ya dhiki chini ya utawala wa Bwana Mubarak, lakini kesi ilikuwa ya haki.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi wa zamani, Habib Al Adly, naye piya amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kuhusika na mauaji ya waandamanaji.
Baada ya hukumu kutolewa kulizuka mtafaruku mahakamani wakati makundi yanayopingana yalipoanza kupigana.
0 Comments