Bao la kwanza kwa timu ya taifa ya Italy lilifungwa kwa njia ya kichwa na mshambuliaji machachari Mario Balotelli kama unavyoona hapo pichani.Ilikuwa furaha sana kwa upande wangu hapo jana.
 Baada ya kufunga goli la kwanza alishangilia sana na kuibusu jezi ya taifa ya timu ya Italy huku wachezaji wa kijerumani wasijue la kufanya.
Haikuwa rahisi kuamini kama kijana Balotelli anaweza kuwazidi akili wajerumani kwa kufunga goli zuri tena baada ya kumzidi ujanja beki wa Ujerumani.
                                                     Goli la pili lilifungwa hiviii
Hapa unaweza kuona kwa mbele vizuri jinsi kijana huyu alivyoweza kuudhibiti mpira na kuachia kombora ambalo kila mmoja alimuonea huruma golikipa wa timu ya taifa ya Ujerumani endapo lingetua mikononi sijui tungesema nini....!!!
Balotelli hakuweza kujizuia kwa kuivua jezi na kutunisha misuli ya mwili wake baada ya kuwaadhibu wajerumani kwa goli la pili.
Mwanadada wa kijerumani bila haya wala makeke aliangusha machozi baada ya kuona Balotelli amethibitisha usemi wake kwamba ``Lazima niwafunge wajerumani na mtanikumbuka kila siku``
Yani hapo mwenye kulia alilia,mwenye kununa alionyesha kununa kwake,kwa kweli jana Ujerumani walionyeshwa kwamba si lolote kwa Italia..mimi nilifurahi sana sijui wenzangu...
Umunthu Umnyama...Agekho ufafanawe Mfwethu...!!! Hakunaga zaidi ya Balotelli...kuna swali? viva Italy n` God yaaa.