Halmashauri ya kijeshi inayoongoza Misri imethibitisha kuwa bunge la nchi limefutwa.
Afisa mkuu kwenye bunge la Misri, aliiambia BBC kwamba amepokea barua kutoka halmashauri ya kijeshi kumuarifu rasmi kuwa bunge limefutwa.
Siku ya Alkhamisi, Mahakama ya Katiba yaliamua kuwa uchaguzi wa bunge uliofanywa mwaka jana ulikwenda kinyume na katiba.
Tangazo hilo limetolewa wakati Wamisri wanapiga kura kumchagua rais mpya atayechukua nafasi ya Hosni Mubarak, ambaye alitolewa madarakani mwaka uliopiota.
Upigaji kura huo wa siku mbili ni wa kuchagua rais kati ya waziri mkuu wa zamani wa Mubarak, Ahmed Shafiq, na Mohamed Morsi wa Muslim Brotherhood.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema inaonesha watu waliojitokeza kupiga kura ni kidogo ikilinganishwa na duru ya kwanza, na vijana wengi wanaonesha wamevunjika moyo na wagombea hao wawili, na hawataki kupiga kura.
0 Comments