Didier Drogba ameziacha klabu mbalimbali na kubwa barani Ulaya na kuamua kusaini
mkataba wa miaka miwili na nusu na klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini
China.
Drogba ambaye amemaliza mkataba na timu yake ya Chelsea mwishoni
mwa msimu uliopita ataungana na aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea Nikolas Anelka
na anatarajia kupokea mshahara wa kiasi cha paundi za Uingereza 200 000 kwa
wiki.
Drogba alisema "Leo nathibitisha ya kuwa nimesaini mkataba wa miaka
miwili na nusu na klabu ya China Shanghai Shenhua. Nitasafiri kuungana na
wenzangu mwezi wa Julai.
"Nimetafakari ofa zote nilizopokewa katika wiki
chache zilizopita, lakini Shanghai Shenhua ni ndio chaguo sahihi kwa wakati
huu".
0 Comments