Mshiriki huyu akiimba kwa hisia kali mbele ya majaji wa EBSS 2012.
Jaji Mkuu wa EBSS 2012 Ritha Paulsen akimpa moyo mshiriki huyu ambae hakupata bahati ya kuchaguliwa lakini hata hivyo alionesha uwezo mkubwa katika kuimba.
Umati wa watu ulifurika katika eneo la Ngome Kongwe kushiriki shindano hilo la aina yake.
Majaji wakifuatilia kwa makini shindano hilo.
Na Mwandishi Wetu
HARAKATI za kupata mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 lililomalizika Jumapili iliyopita kisiwani Zanzibar limeacha gumzo kubwa kisiwani humo.
Shindano hilo linaloanza kwakuzunguka mikoani kutafuta vipaji na hatimaye kuvileta Dar es Salaam, lilikuwa limetokea Dodoma, ambako pia majaji walikiri kuwa kulikuwa na ushindani mkubwa sana katika kuwapata washindi.
‘Mwaka huu kumekuwa na ushindani mkubwa sana toka tumeanzisha shindano hili kama miaka mitano iliyopita’ anasema jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen.
Mwaka huu shindano hilo linadhamiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Zantel ambalo litatoa milioni hamsini kwa mshindi pamoja na mkataba wa kurekodi.
Huku washiriki wa Dodoma wakiwa wameshapatikana, ilikuwa zamu ya Zanzibar wikiendi hii, ambako baada ya wawakilishi wa Zanzibar kutangazwa kuliibuka shangwe kubwa, huku wengi wakiangusha vilio baada ya kukosa nafasi.
Kati ya vijana zaidi ya mia nne wa kizanzibar waliuokuwa wamejitokeza kwa siku mbili mfululizo kutaka kupata nafasi kwenye shindano hilo kubwa zaidi Tanzania, walipatikana vijana watano.
‘Zanzibar imekuwa ya kipekee, na tumepata washindi watano, wakike watatu na wakiume wawili, tofauti na mikoa mingine’ anasema Master J, mmoja wa majaji.
Mmoja kati ya majaji wa shindano hilo ambae alikuwa kivutio kikubwa ni jaji Salama Jabir ambae alikuwa akiwavutia vijana wengi wa kisiwani hapa waliotaka kupiga nae picha muda wote.
Wengine walisikika wakimuomba asiwakosoe sana pindi watakapoanza kuimba mbele ya majaji.
“Mimi nakwambia wewe Salama kwanza ujue kuwa ni mkazi wa huku kwetu na pia basi usitubanie sana tafadhali kwa kuwa wengine kuimba twajua ila ni masuala madogomadogo tu” alisema kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Hassan.
Hata ilipofika zamu ya kuanza kusikilizwa mshiriki mmoja mmoja wale waliokuwa wameenda kushiriki wakiwa wamebeba vyombo mbalimbali vya muziki walijikuta wakikosa kwa kuwa walionesha zaidi umahiri katika kutumia vyombo hivyo badala ya kuonesha uwezo wao katika kuimba.
Gumzo lilolobakia kisiwani hapa hususan kwa vijana wengi ni walikuwa wakijiuliza iweje wasichana wameweza kufanya vema zaidi na kuwaridhisha majaji zaidi ya wavulana.
Naye Jaji Mkuu wa EBSS Ritha Paulsen alisema kuwa ana imani kuwa mwaka huu washindi watakuwa na uwezo mkubwa wa kuimba kwa na hilo limejidhihirisha katika usaili wa Zanzibar.
Jumamosi ijayo EBSS itaamia mkoani Lindi kwa kutafuta vipaji.




0 Comments