Haya ni Maoni ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kupitia Wall ya Facebook yake.
“Kimsingi bajeti inapopelekwa Bungeni na serikali inakwenda kwa ajili ya mjadala na marekebisho palipo na mapungufu NA SI KUPITISHWA KAMA WAJIBU TU, tunategemea mjadala wenye lengo la kiboresha kwa faida ya wananchi. Sasa haya malalamiko ya baadhi ya wabunge barabarani, mara ” niko tayari kufukuzwa”!! Nani anamfukuza nani?!
Nani anayetishia uhuru, haki na wajibu wa kikatiba wa wabunge wetu mpaka wanalalamika barabarani?!! Nashauri wabunge timizeni wajibu wenu, jadilini na kuishauri serikali ndani ya bunge juu ya maboresho ya bajeti iliyoletwa kwenu!”
0 Comments