Kulia ni Katibu wa Taasisi za Kiislam Sheikh Ponda Issa Ponda nakushoto ni Suleiman Khamis anayehusika na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa mataifa. Katikati ni Mratibu wa Fedha wa Al-Mallid Propagation Centre(International) Rajab Katimba.



Na.MO BLOG TEAM
Jumuiya na Taasisi za kiislam nchini Tanzania imeendelea kusisitiza na kuitaka serikali kuunda tume huru kulichunguza Baraza la Mitihani na kufanya marekebisho haraka ikiwemo kumwajibisha mara moja Katibu Mtendaji wa baraza la Mitihani Dkt. Joyce Ndalichako.
Taarifa hiyo imesema hatua hiyo ilithibitisha madai ya Wakuu wa Shule za Kiislam kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwa matokeo ya awali yalikuwa yamechakachuliwa.
Imefafanua kuwa wakati Wizara ya Elimu imekaa kimya juu ya madai yao, ushahidi umezidi kupatikana juu ya utendaji usiokuwa makini wa Baraza la Mitihani.
Ushahidi mwingine kuonesha uozo wa Baraza la Mitihani ni pale ilipogundulika kwamba kuna mwanafunzi ambaye hakufanya mtihani kabisa lakini alipewa.
Mwanafunzo huyo anaitwa Mariam A. Nyembo mwenye namba S 01888/0509.
Matokeo ya mwanafunzi huyo yamerekebishwa hivi karibuni baada ya Mkuu wake wa Shule kupeleka malalamiko Baraza la Mitihani.
Taarifa hiyo imesema ni wazi kuwa kwa utaratibu huo wa Baraza, wanafunzi wote wamekuwa wakidhulumiwa kwa kupimwa kwa vigezo ambavyo wao na waalimu wao hawavijui.