Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Mhe. John Mnyika ametolewa nje ya bunge muda huu na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kukataa kufuta kauli yake kuwa Rais Kikwete ni dhaifu wakati alipotakiwa kufanya hivyo. Mnyika ametolewa nje ya bunge wakati wabunge wakichangia mjadala wa bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni. Mnyika atarudi bungeni kesho saa tatu asubuhi.
0 Comments