Mkurugenzi wa Idara ya Kupambana na Madawa ya Kulevya na Kurekebisha tabia Ahmed Awadh Salim akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji aliekushoto yake katika maadhimisho ya Siku ya kupiga vita Madawa ya Kulevya hapo Acrotanal mjini Unguja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji akitoa hotuba ya Ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya kupiga vita Madawa ya Kulevya hapo Acrotanal mjini Unguja.

Baadhi ya Vijana waliokuwa wakitumia madawa ya Kulevya ambao kwa sasa wameacha madawa hayo na kujishughulisha na kazi mbali mbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji hayupo pichani katika maadhimisho ya Siku ya kupiga vita Madawa ya Kulevya hapo Acrotanal mjini Unguja. 
Vijana waliokuwa wameathirika na Utumiaji wa Madawa ya kulevya wakicheza mchezo wa kuigiza namna ya mtu akimia madawa ya kulevya na kuweza kujikinga na utumiaji wa madawa hayo katika Ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya kupiga vita Madawa ya Kulevya hapo Acrotanal mjini Unguja. PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR