Na Mwandishi Wetu

WAREMBO wanaotarajiwakushiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012  jumamosi  hii wanatarajiwa kutembeleamakumbusho ya Taifa kwa ajili ya kujifunza.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi huowa Makumbusho ya Taifa uliopo mkatabala na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM)Juni, 22 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hiloDina Ismail, alisema ziara hiyo itawasaidia sana warembo hao katika harakati zao zakielimu.

Alisema Makumbusho ya Taifani sehemu muhimu kwa kila Mtanzania kufahamu kutokana na kuwepo vitu vingi vyakihistoria vilivyopata kutokea katika karne zilizopita.

“Kamamjuavyo kule kuna kuna fuvu la mtu wa kwanza duniani (zinjathropas), vyombo,magari na vitu vingine vya kwanza kuanza kutumika,”alisema.

Dina aliongeza kuwamaandalizi kwa ajili ya shindano hiloyanakwenda vema ambapo washiriki 13 kutoka vyuo vya IFM, Ustawi wa Jamii, ChuoCha Biashara (CBE), uandishi wa Habari (DSJ) na Huria (OUT) wanaendelea namazoezi kwenye hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar esSalaam.

Warembo hao ambao wapo chiniya ukufunzi Marlydia Boniface na Bob Rich ni  pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi,Nancy Maganga, Hilda  Edward, DianaNyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim,Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.

Shindano hilo limedhaminiwana Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s Original, DodomaWine, Ndege Insurance, Shear Illusions, Skylight Band, Lamada Hotel, ScreenMasters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fmna blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.