Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi ameanzisha rasmi safari ya kupanda mlima kilimanjaro kwa mwaka huu inayoratibiwa kila mwaka na kampuni ya Geita Gold Mining LTD. Kampeni hiyo ya mapambano dhidi ya Ukimwi na maambukizi ya Ukimwi aliyoanza nayo Mzee Mwinyi tangu mwaka 2002 na inafahamika kama Kilimanjaro Climb against HIV/AIDS 2012 Mzee Mwinyi alifanya uzinduzi huo katika lango la Machame lililoko wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.-Kilichovutia zaidi ni kwa Mzee Ruksa kuwa fit kwa kipande alichotembea na leo kwa kiasi fulani alipunguza ule umbali anaopanda ambapo kila mwaka usababisha kati ya kundi lake la wapambe robo tatu kuishia njianiPichani Mzee Mwinyi pamoja na Mkewe Mama Siti Mwinyi wakiongozana na mwenyeji wao mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Novatus Makunga pamoja na kundi la Wapanda Mlima.