Serikali ya Uturuki inafikiri kuwa ndege yake moja ya kijeshi iliyodunguliwa na
Syria Ijumaa, pengine iliingia katika anga ya Syria.
Rais Abdullah Gul, aliliambia shirika la habari la Uturuki, Anatolia, kwamba
ni kawaida kwa ndege za kijeshi kuvuka mipaka ya nchi, zinaposafiri kwa
kasi.
Bwana Gul alisema serikali yake inawasiliana na Syria kuhusu tukio hilo.
Majeshi ya wanamaji ya nchi zote mbili yanafanya msako wa pamoja kuwatafuta
marubani wa ndege hiyo.
Uturuki ilimundosha balozi wake nchini Syria mwezi wa March baada ya ghasia
kuzidi nchini humo, lakini Bwana Gul alisema hiyo haizuwii serikali yake
kuwasiliana na serikali ya mjini Damascus.
0 Comments