Rais Mahamadou Issoufou wa Niger amesema kuwa wapiganaji wa Jihad kutoka Afghanistan na Pakistan wanapata mafunzo kutoka kwa makundi ya makundi ya wanamgambo nchini Mali.
Rais huyo amekaririwa akisema kuwa nchi yake ina habari kuwa kuna wanamgambo wanaendesha mafunzo Kaskazini mwa nchi hiyo.
Aidha ameliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha azimio linalokubalia kuingiliwa kijeshi nchini Mali ikiwa mazungumzo ya amani yatakwama.