Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi Mhe. Mohamed Abdelaziz leo asubuhi.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuonesha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi Mhe. Mohamed Abdelaziz picha ya waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Karume wakibadilishana hati za muungano muda mfupi baada ya Rais Kikwete na mgeni wake kumaliza mazungumzo rasmi ikulu jijini Dar es Salaam leo. Mhe. Mohamed Abdelaziz Rais wa Jamhuri ya kiarabu ya Sahrawi aliwasili nchini jana jioni kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
(Picha na Freddy Maro-IKULU)