Jamaa zaa waliouawa kwenye shambulio la kujitoa mhanga |
Kumetokea shambulizi la bomu la kujitolea mhanga katika makao makuu ya polisi kaskazini mwa Nigeria.
Maafisa wa polisi wameripotiwa watu kadhaa kuuawa lakini idadi halisi ya waliouawa haijulikani.
Kufuatia shambulio hili, vikosi vya usalama mjini humo vilifanya msako katika maficho ya kundi la haramu la Boko Haram na kusababisha ufyatulianaji mbaya wa risasi, hii ni kwa mujibu wa duru za polisi.
Kwa sasa ulinzi umedhibitiwa sana mjini Maiduguri, ambao ni ngome ya ya kundi hilo.
Hata hivyo hakuna kundi lolote limedai kufanya shambulio hilo.
Aidha Boko Haram - ambalo jina hilo lina maanisha "tunapinga sera za kimagharibi" limekuwa likilenga vituo vya polisi kwa mashambulizi, shule na majengo mengine ya serikali kwa takriban sasa miezi 21.
Kundi hilo linataka sheria ya kiisilamu kutumika kote nchini Nigeria.
Inaarifiwa watu watano wamefariki wakiwemo, mshambuliaji mwenyewe, polisi na raia watatu, kulingana na polisi wa eneo la Maiduguri.
Kwa jumla watu kumi na mbili wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo.
Kundi la Boko Haram lilianza kusifika mwaka 2009 wakati mamia ya wafuasi wake waliuawa waliposhambulia vituo vya polisi mjini Maiduguri.
Mwanzilishi wa kundi hilo, Mohammed Yusuf, alikamatwa ingawa alifariki akiwa angali amezuiliwa.
Mwaka 2010 kundi hilo lilianza kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya taasisi za serikali.
Mwaka jana kundi hilo lilifanya mashambulizi ya kujitoa mhanga dhidi ya makao makuu ya umoja wa mataifa na yale ya polisi mjini Abuja mwaka jana.
BBC
0 Comments