Baadhi ya warembo watakaoshiriki shindano la Miss Dar Inter College 2012 wakimsikiliza mwalimu wao Marlydia Boniface wakati wa mazoezi yao jana kwenye hoteli ya Grand Villa.
Baadhi ya warembo watakaoshiriki shindano la Miss Dar Inter College 2012 wakimsikiliza mwalimu wao Marlydia Boniface wakati wa mazoezi yao jana kwenye hoteli ya Grand Villa.
Na Mwandishi Wetu
WAKATI shindano la kumsaka Miss DarIntercollege 2012 likitarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho yaTaifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) duka la vipodozi laShear Illusions,pamoja na mbunifu maarufu wa mavazi,Mustafa Hassanali wamejitosakudhamini shindano hilo .
Awali shindano hilolilipangwa kufanyika juni 8 kabla ya kusogezwa mbele kutokana na sababumbalimbali ikiwemo baadhi ya warembo kuwa katika mitihani pamoja na mafunzo yao kwa vitendo ‘Field’.
Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alimesema kwambaShear lenye matawi yake jengo la Millennium Tower na Mlimani City linajihushana uuzaji wa vipodozi halisi ‘original’ kutoka nje ya nchi litatoa vipodozi kwawarembo watakaoshiriki,huku Hassanali atatoa zawadi ya magauni ya warembo.
Alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea ambapo leo warembo hao ambao awaliwalikuwa wakifanya mazoezi kwenye hoteli ya Lamada, jana walihamishia kambi yao kwenye hoteli yaGrand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Dina ameongeza kuwa mpaka sasa wameshapatikanawarembo 13 ambao wapo chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upandewa shoo wakinolewa na dansa aliyepata kufanya vema miaka ya nyuma, Bob Rich.
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja yawarembo kutoka Miss Dar Intercollegeanafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu huria (OUTambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wamwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja naVeronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, DianaNyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim,Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya BiaTanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, SkylightBand,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, GrandVilla Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwaMtaa na Fullshangwe.
mwisho
0 Comments