Promota wa ukweli King James wa Den Haag nchini Holland akipokea tabasamu la ukweli toka kwa msanii wetu anayetamba hivi sasa pande za Afrika mashariki na ya kati bidada Isha Mashauzi hivi majuzi alipotumbuiza Den Haag.King James anawashukuru watu wote waliojumuika nae katika kumpa sapoti ukumbini hapo na pia anawashukuru hata wasiobahatika kufika ukumbini hapo kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao.Akizungumza na Maganga One Blog King James anasema hana cha kuwalipa ila amefurahishwa  sana na kuja kwenu ukumbini.
Mke wa Promota King James Mrs Trianna James kushoto,Aunt wa Isha Mashuzi mwenye gauni jekundu na Isha Mashauzi wakipata picha ya pamoja.Mke wa James pia ametoa shukrani za dhati kwa mashoga zake woote waliofika ukumbini kwa kuwapa sapoti.
Palikuwa hapatoshi hapooo..yani mzuka juu ya mzuka... ni Isha Mashauzi akiwa na wapenzi wake wakiselebuka kwa pamoja.King James anawashukuru sana watu wake wote mliokuja ukumbini.
Picha ya kumbukumbu kwa mashabiki waliofika ukumbini hapo kumshuhudia Isha Mashauzi.King James anawashukuru sana nyote mliofika ukumbini siku ile ya show.
Toka kushoto ni bidada Isha Mashauzi,bidada Sekky na bint James Biboze wakipata kumbukumbu siku ya show ya Isha Mashauzi nchini Holland siku za hivi karibuni.King James na mkewe wanawashukuru sana kwa kampani yenu kwa kuja kwenu ukumbini.
Hiki ni kikosi kazi ambacho nacho hakikubaki nyuma siku ya show.King James anawapa Big up kwa ujio wenu ukumbini siku hiyo.
Dj Khatib akiwa amempakata mkewe huku Isha Mashauzi akilamba picha kuweka kumbukumbu na mashabiki wake.King James anawashukuru sana kwa ujio wenu pale ukumbini.
Wakati show ikiendelea huku mashabiki walikuwa makini kumsikiliza bidada Isha jinsi alivyokuwa akitumbuiza ukumbini pale.King James anawashukuru sana kwa ujio wenu pale ukumbini.
     Kushoto ni mke wa Promota na kulia ni mke wa Dj......Hongereni mlipendeza.
Wacha weeeee...!!! show ilikuwa bab kubwa..hongera King James kwa kufanikisha mpango mzima wa kumleta bidada Isha Mashauzi Den Haag.King James anawashukuru sana wale woote walioweza kufanikisha shughuli nzima na mashabiki wote waliompa sapoti,anasema bila nyinyi show isingeweza kuwepo..ni vigumu kumshukuru kila mmoja kwa majina ila anawashukuru sana tena sana.