Mkurugenzi wa kikundi cha uigizaji cha The Original Comedy, Isaya Mwakilasa 'Wakuvanga' akielezea katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, jinsi walivyojiandaa kushiriki katika Bonanza la Tigo litakalofanyika leo  na kesho kwenye ufukwe wa Coco, Oysterbay jijini. Kushoto ni Mratibu wa Promosheni wa Tigo, Edward Shila na Alice Maro ambaye ni Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)