Jamii ya watu wanaoishi maeneo ya vijijji barani Afrika sasa wanaweza kuboresha huduma ya maji kwa kutumia teknolojia ya simu ya mkononi.
Kundi la wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wametengeneza kifaa maalum ambacho kitawekwa kwenye pampu ya kuvuta maji.

Kifaa hicho kinaweza kutuma ujumbe wa maandishi kwenye simu ya mkononi kama kuna tatizo linaloweza kujitokeza.
Kwa kuanzi kifaa hicho kinatarajiwa kufanyiwa majaribio katika vijiji vipatavyo 70 nchini Kenya na kuna matumaini kwamba kitawezesha kurahisisha matengezo ya mitambo ya kusambaza maji.