Wabunge karibu 10 nchini Zimbabwe wametahiriwa kama moja wapo
ya hatua zao ya kukabiliana na kusambaa kwa virisi vya Ukimwi nchini humo,
Nje ya majengo ya bunge mjini Harare , kulijengwa zahanati ndogo kwa sababu
ya shuhuli hizo za kuwapasha wabunge tohara.
Blessing Chebundo, ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wanaopambana na Ukimwi
amesema nia yake hasa ya yeye kuamua kupashwa tohara ni kuchochea wanaume nchini
Zimbabwe kutahiriwa.
Bwana Chebundo anasema kuna wabunge zaidi ya 120 na wafanyikazi wa bungeni
ambao wameonyesha nia yao ya kutahiriwa.
Shirika la afya duniani WHO linasema kupasha tohara kunapunguza hatari ya
wanaume kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60.
Zimbabwe ni moja wapo wa mataifa 13 barani Afrika ambapo mwaka wa 2007
shirika la WHO inasema kuna haja kubwa ya kuanzisha harakati za kuwatahiri
wanaume.
Jana, wabunge hao walijitokeza hadharani ili kupimwa hali yao ya Ukimwi.
Wabunge hao wanachochea wanaume nchini Zimbabwe kukubali kutahiriwa, kama
njia mojawapo ya kupumguzu maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Hii nikutokana na takwimu za hivi karibuni zinazoonyesha kuwa karibu robo ya
wanaume wote nchini Zimbabwe wameambukizwa virusi. |
0 Comments